Baada
ya kivuko cha MV Kilombero kuzama Januari, 27 mwaka hu na kusababisha
kusimama kwa huduma ya kivuko kwenye Mto Kilombero Mkoani Morogoro
kimeanza kufanyakazi rasmi tarehe 29 Februari, 2016 mara baada ya
kukamilika kwa ukarabati wake.
Katika
taarifa imeyotolewa na Wizara ya Ujenzi imeeleza kuwa kivuko hicho
kinaendelea na ratiba yake ya utoaji huduma ya kivuko kuanzia saa 12:30
asubuhi hadi saa 1:00 jioni kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment