Siku
tatu baada ya mwandishi wa Mwananchi na DW, Salma Said kutoweka, jana
alipatikana baada ya kukutwa katika Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam na kupelekwa kituo kikuu cha polisi kuhojiwa.
Habari
zilizopatikana jana jioni na kuthibitishwa na mumewe, Ali Salim Khamis
na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi, Simon Siro zilisema Salma
alisajiliwa jana mchana katika hospitali hiyo.
Ali
aliyekuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alisema kwa
ufupi kuwa amepata taarifa hizo na kufika Dar es Salaam kuzifuatilia.
Kamanda
Siro alisema ni kweli Salma amepatikana na ametumwa mkuu wa upelelezi
wa kanda hiyo kumfuata hospitali ampeleke kituoni kwa mahojiano.
“ Tumefungua jalada la uchunguzi wa tukio hili juzi,” alisema Sirro na kuongeza.
“ Tumefungua jalada la uchunguzi wa tukio hili juzi,” alisema Sirro na kuongeza.
“Wapelelezi
walizungumza na mume wa Salma na kuna mambo amewaeleza lakini hatuwezi
kuyaweka wazi kwa sasa, hadi uchunguzi utakapokamilika, tumeipata namba
ya simu aliyowasiliana nayo na mumewe akiwa huko kunakoaminika
amefichwa,” alisema.
Wakati
huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika tamko lake ililolitoa
jana ilieleza kuwa kutekwa kwa mwanahabari huyo kumezua maswali mengi
kwa wananchi, familia yake, wadau na wanahabari wa ndani ya nchi na wale
wa jumuia za kimataifa.
“Kutekwa
kwa Salma kunatokana na kazi yake ya uanahabari, ndiyo maana ushahidi
wa awali uliopatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti
inayoaminika kuwa ni yake, ulieleza wazi kutekwa kwake kunatokana na
yeye kuripoti dosari zinazoendelea katika uchaguzi wa marudio Zanzibar,” alisema Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Kambi ya Upinzani.
Mbilinyi
ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) alidai kuwa matukio
mbalimbali yanayoendelea Zanzibar yakiwamo ya matumizi ya nguvu, vitisho
na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea
kuitia Serikali ya CCM doa, Taifa na dunia nzima.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment