Wakati polisi visiwani Zanzibar wakimhoji Naibu Katibu Mkuu wa CUF,
Nassor Ahmed Mazrui jana, ulinzi uliimarishwa mjini Unguja huku askari
wenye silaha na magari ya deraya wakifanya doria mitaani.
Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda.
Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda.
Barabara
zinazoelekea makao makuu ya polisi kutokea Jang’ombe, Kilimani na
Bomani zilifungwa huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiwa vimetapakaa
maeneo hayo na mitaa mbalimbali mjini Unguja.
Wakazi wa Zanzibar
wanaojiandaa kwa uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20,
kuanzia Jumatano mchana walishuhudia askari wenye sare wakiwa katika
magari maalumu ya kijeshi wakirandaranda kwenye barabara za Unguja,
hususan mitaa ya Ng’ambo kupitia Mnazi Mmoja, Darajani, Amani, Chumbuni
na Mtoni kuelekea Bububu.
Wakati hali
ikionekana hivyo mitaani, Mazrui alikuwa ndani ya Ofisi ya Upelelezi ya
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani mjini Unguja ambamo alihojiwa kwa
saa tatu na nusu.
Alianza kuhojiwa tangu saa 2.00 asubuhi kama
alivyotakiwa na jeshi hilo kuripoti kupitia barua ya wito aliyotumiwa
hivi karibuni, hadi saa 5.30
Hata baada ya kumaliza kuhojiwa, Mazrui
aliyekuwa waziri wa biashara, alilazimika kubaki kituoni hapo akisubiri
kukamilika kwa taratibu za dhamana. Aliruhusiwa kuondoka saa 6.40
mchana.
Pamoja na ulinzi kuimarishwa, mamia ya wananchi, hasa
wapenzi, wanachama na wafuasi wa CUF, walifika makao makuu ya chama
hicho yaliyoko Mtendeni ili kumpokea Mazrui akitokea polisi.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mazrui alisema alihojiwa na
polisi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa Dunga Kiembeni,
Wilaya ya Kati mkoani Kusini Unguja kwamba chama chake cha CUF
kimechoshwa na vitendo vya hujuma na vya kihuni dhidi ya mali na ofisi
zao.
“Naam, nimewaambia kwamba hiyo ni kauli yangu na niliyesema
hayo ni mimi kuwa CUF tumechoshwa na uhuni huo,” alisisitiza Mazrui
mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti ya kuwa na wadhamini
wawili na kila mmoja wao kutakiwa kuweka hapo Sh500,000.
0 comments:
Post a Comment