newspointtz blog
Wasichana
wanaovaa nguo fupi za kubana na wavulana wanaovaa milegezo jijini
Mbeya , juzi walipata wakati mgumu baada kundi la vijana kuwavua nguo
zao na kuzichana hadharani, kutokana na gari la matangazo kupita jijini
hapa likiwataka watu kuvaa nguo za heshima zinazoendana na maeneo
husika.
Tangu
Machi 7 hadi 9, gari la matangazo ya Kampuni ya Studio H ya Huruma
lilipita mitaa mbalimbali ya jijini Mbeya, likiwataka wasichana kuacha
kuvaa vimini na vijana kuacha kuvaa mlegezo.
Baada
ya tangazo hilo, vijana walianza kuwavamia wasichana na wavulana
waliovaa milegezo maeneo ya Uyole, Soweto, Kabwe na Mwanjelwa, huku
wanawake waliokuwa wakiuza matunda wakiwarushia vitenge wasichana
waliochaniwa nguo ili wajisitiri.
Ofisa Habari Jiji la Mbeya, John Kilua alisema uongozi hauhusiki na tangazo hilo.
Hata
hivyo, Ofisa wa Kampuni ya Studio H ya Huruma, Siyata Mbua alisema
walitoa tangazo hilo baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya jiji
na kampuni yake.
Mbua
alisema kazi ya kuzuia nguo zisizo za heshma inahusu Serikali, lakini
kampuni iliamua kujitolea kwa makubaliano na jiji kwa mwaka mmoja.
“Lengo
ni kuwahamasisha wananchi wavae nguzo za heshima. Hatuwahamasishi
vijana wawavamie watu, bali tunawataka kila mmoja avae nguo kulingana na
maeneo anayofanyia kazi,”alisema. Mabua alisema lengo ni kuelimishana zaidi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema hajapata malalamiko na
kuwataka vijana kuheshimu utu wao kwa kuvaa nguo za heshima.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment