Michel Platini, aambaye ni kapteni wa zamani wa Ufaransa anataka
kugeuza uamuzi wa shirikisho la soka duniani FIFA kumpiga marufuku ya
miaka sita kwa kupokea malipo ya dola ilioni mbili kutoka kwa Sepp
Blatter.
Ni hatua ya mwisho kwa Michel Platini, ambaye bado ni mkuu rasmi wa UEFA ukisubiriwa uamuzi wa rufaa hiyo.
Ameiomba mahakama hiyo ya Uswizi kutupilia mbali marufuku hiyo ya miaka sita iliyopunguzwa hivi karibuni na FIFA kutoka miaka 8.
Na anataka uamuzi utolewe kabla ya michuano ya ubingwa wa Ulaya nchini Ufaransa inayoanza Juni.
Alihusika pakuu katika uandalizi wa mashindano hayo nyumbani na ana hamu kubwa kuyahudhuria.
Ameendelea kusisitiza kuwa pesa hizo za dola milioni mbili alizopewa
na mkuu wa zamani wa FIFA zilikuwa ni malipo ya kazi ya ushauri aliotoa
miaka tisa iliyopita na ni za halali kwasabau kulikuwana makubaliano ya
mdomo.
Sepp Blatter, anakabiliwa na marufuku ya miaka sita kuhusu
suala lilo hilo anatarajiwa pia kuwasilisha kesi yake mbele ya mahakama
hiyo inayotoa uamuzi wa mwisho kuhusu mizozo aina hiyo.
Aliyekuwa
naibu wa Michel Platini katika UEFA, Gianni Infantino amechaguliwa rais
wa FIFA ijumaa iliyopita hatua iliyoacha pengo katika uongozi wa
shirikisho hilo la soka Ulaya miezi michache kabla ya kuidhinishwa kwa
mara ya kwanza michuano yake
Chanzo:bbc
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment