RAIS John Magufuli amesema anatamani
mafanikio ya nchi ya Vietnam kiuchumi na kubainisha kuwa ziara ya Rais
wa nchi hiyo, Truong Tang Sang nchini, ni fursa na changamoto kwa
watanzania kujifunza mambo mengi, yatakayosaidia kukuza pia uchumi wa
Tanzania.
Aidha amehamasisha Watanzania
kuchangamkia fursa na rasilimali zilizopo nchini katika kujiinua na
kuimarisha nchi yao kiuchumi. Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi
tajiri kwa rasilimali na fursa nyingi, ingawa bado iko nyuma
kimaendeleo.
Kwa upande wake, Rais Sang amesema nchi yake na Tanzania
zimekubaliana kushirikiana katika maeneo ya biashara, kilimo, viwanda na
uvuvi lengo likiwa ni kuhakikisha nchi zote zinanufaika kwenye
ushirikiano huo.
Akizungumza
katika mkutano wa waandishi wa habari na marais hao Ikulu Dar es Salaam
jana, Dk John Magufuli alisema ni wakati sasa wa Tanzania kujifunza
kutoka kwa nchi hiyo ya Vietnam ambayo pamoja na kukabiliwa na vita ya
muda mrefu, imefanikiwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati.
“Ukweli ni kwamba ziara ya Rais Sang nchini kwetu ni muhimu sana na
imekuja kwa wakati muafaka.
Mwaka 1976 Rais wa Vietnam alikuja
nchini na alichukua mbegu ya korosho na kuipeleka nchini kwake, na leo
hii Vietnam ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuzalisha korosho duniani,”
alisema. Alitaja mafanikio mengine ya nchi hiyo ni pamoja na kuwa na
uchumi wa kati, licha ya kukabiliwa na mapigano ya muda mrefu. Ilipata
uhuru wake mwaka 1945 na ilidumu kwenye mapigano hadi Julai 2, mwaka
1976.
Alisema mwaka 1977 mapato ya kila raia
wake yalikuwa ni dola 100, lakini sasa imefanikiwa kupandisha mapato
hayo na sasa kila raia wa nchi hiyo mapato yake ni dola 2000 kwa mwaka
na imepunguza kiwango cha umasikini kwa asilimia 50. “Sisi tangu mwaka
1960 bado tuko kwenye nchi masikini, kwa hiyo hii ni changamoto kwa nchi
yetu. Tunatakiwa kujifunza kuondokana na hali hii.
Wao uzalishaji kwa mchele wanalima mara
tatu kwa mwaka, sisi tunalima mara moja tu na inawezekana uzalishaji
wetu ni mdogo sana,” alisema. Alisema nchi hiyo pamoja na kuchukua mbegu
ya korosho nchini, ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha korosho duniani,
wakati Tanzania ndio iliyotoa mbegu hiyo, zao hilo badala ya kuzalishwa
kwa wingi ndio uzalishaji wake unafifia.
“Samaki sina uhakika kama walichukua
huku, lakini leo hii Vietnam ni wazalishaji wa samaki wakubwa sana.
Lakini kwa nchi yetu ambayo ina maziwa 21 na mito kila mahali na bahari
lakini uzalishaji wa samaki uko chini…” “Tuna ng’ombe zaidi ya bilioni
22 hadi bilioni 23 nafikiri tunaweza kuwa wa pili barani Afrika baada ya
Ethiopia, lakini ngozi zetu za viatu hapa tunaagiza nje.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
RAIS MAGUFULI AITAMANI VIETNAM
Reviewed by Newspointtz
on
08:05:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment