Sababu 5 DORTMUND VS BAYERN MUNICH NI 50% VS 50%
Zimesalia mechi takribani kumi kwenye ligi ya bunsesliga, leo tutaona mchezo mgumu ambao unakutanisha timu mbili ambazo zipo juu ya msimamo wa ligi. Borussia Dortmund chini Kocha Thomas Tuchel watawakaribisha Bayern Munich ya Pep Guardiola kwenye dimba la Signa Iduna Park.
Ni mechi ngumu kutabiri matokeo, hiyo ni kutokana na ubora wa timu zote mbili pamoja na matokeo mazuri wanayopata kwenye ligi ya bundesliga. Nje ya uwanja unaweza kutoa asimilia 50% kwa kila timu kushinda kutokana na sababu tofauti tofauti.
Kwanza pengo la pointi baina yao ndio kitu kinachoongeza mvuto wa mechi hii, baada ya Bayern kupoteza mechi ya mwisho katikati ya wiki dhidi ya Mainz kwa mabao 2-1 kisha Dortmund kushinda 2-0 dhidi ya SV Darmstadt tofauti kati yao ni point 5 tu Bayern wakiwa na 62 huku Dortmund 57.
Hivyo Dortmund wanataka kupunguza pengo zaidi hadi kufika point 2 wakati Bayern wanataka kuongeza kuelekea kutwaa taji la tatu mfululizo la bundesliga
Pili matatizo ya safu ya ulinzi, Dortmund wanamkosa beki wake wa kati Sokratis wakati Bayern itawakosa Jerome boateng, Javi Martinez na Holder Badstuber. Hivyo kitendo cha kumtumia kiungo sven Bender kucheza na Hummels kinaweza kusababisha makosa ambayo yanaweza kutumiwa na safu ya ushambuliaji ya Bayern
Pia Bayern kumtumia David Alaba kunatoa nafasi kwa safu ya ushambuliaji ya Dortmund kung’ara kwenye mchezo huu sababu ni kwamba David Alaba hafanyi vizuri sana anapotumika kama mlinzi wa katikati.
Tatu uwepo wa safu bora za ushambuliaji kwa timu zote mbili pia kinachangia ugumu wa mechi hii. Bayern watamtegemea mshambuliaji Robert Lewandowski mwenye goli 23 huku akipata msaada kutoka kwa Arjern Robben, Thomas Muller na Deogratius Costa. Lakini pia Dortmund wana Pierre Emerick Aubameyang mwenye golii 22 huku akisaidiwa na Marco Reus na Henrikh Mikhitaryan ambao walipumzishwa katikati ya wiki.
Hivyo ukiondoa vita kati ya Bayern na Dortmund pia bado kuna vita ya ufungaji bora inayoendelea kati ya Lewandowski na Aubameyang.
Nne, Dortmund wanabebwa na rekodi yao nzuri ya hivi karibuni kushinda mechi za nyumbani. Wemeshinda mechi saba karibuni za bundesliga kwenye uwanja wa signal Iduna Park
Tano, Bayern pia wanajivunia rekodi nzuri waliyonayo dhidi ya Dortmund kwenye mechi za karibuni ndani ya mashindani yote. Kwenye mechi sita za karibuni Bayern wameshinda nne na Dortmund kushinda mbili
Ni mechi ngumu kuitabiri lakini kuna uwezekano wa kuisha kwa sare, tusubiri tuone muda mfupi ujao.
0 comments:
Post a Comment