SERIKALI inatarajia kuunda Mamlaka Kuu
ya Mapato ya Taifa nje ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) iliyopo
sasa, kuondokana na malalamiko ya kero za kodi kwa wananchi wenye kipato
cha chini.
Aidha, TRA imefuta kodi elekezi kwa
bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi hususani zinazotoka
China, hivyo wafanyabiashara waliokuwa wakinufaika na fursa hiyo,
watatakiwa kuanza kulipa kodi.
Hayo yalielezwa jijini Dar es Salaam
jana na Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari. Akizungumzia mamlaka mpya itakayoanzishwa,
alisema hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kusaidia wananchi wa kipato
cha chini, kumudu kulipa kiwango cha kodi kinachowekwa na mamlaka hiyo.
“Napenda kuwaambia umma wa Watanzania
kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inawajali watu wake na ndiyo maana
imeona kuwa kuna haja ya kuunda mamlaka moja ya utozaji wa kodi
itakayojumuisha taasisi zote zinazohusika na kukusanya mapato nje ya
kodi na ushuru ili kuondokana na malalamiko mengi ya wananchi juu ya
utozaji wa kodi hasa katika halmashauri zetu,” alisema Kidata.
Kamishna Kidata alisema katika dunia,
hakuna serikali ambayo imechaguliwa na wananchi ikaamua kuwakandamiza
wananchi wake . “Hivyo basi kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa
kuunda mamlaka hiyo ambayo itasaidia kuweka viwango vya kodi ambavyo
wananchi wa hali ya chini watamudu kulipa kutokana na biashara au kazi
wanazozifanya,” alisema.
Kamishna huyo alisema mamlaka yake kwa
kushirikiana na mamlaka nyingine, zinazokusanya kodi katika halmashauri
nchini, watahakikisha wanapatia ufumbuzi kero ya kodi kwa wananchi wa
hali ya chini kwa kupata muafaka, ambao utasaidia pande zote mbili bila
kukandamiza upande wowote ama Serikali au mwananchi wa kawaida.
Ingawa TRA imekuwa na rekodi nzuri ya
ukusanyaji wa kodi, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi
kuhusu kodi zinazodaiwa kuwa za kero. Akizungumzia kufutwa kwa kodi
elekezi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kwa msamaha wa kodi, Kaimu
Kamishna Kidata alisema awali, kulikuwa na punguzo la kodi kwa
wafanyabiashara wanaoagiza na kuingiza bidhaa kutoka China kwa
kupunguziwa sehemu ya kodi.
“Tumeamua kuondoa kodi elekezi kwa
sababu haina faida kwa taifa letu kwani inawanyima wafanyabiashara
wengine ambao hawaagizi bidhaa kutoka China, fursa ya kushindana
kibiashara.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
SERIKALI KUJA NA TRA MPYA MAALUMU
Reviewed by Newspointtz
on
10:34:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment