NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

UEFA LEO Messi, Aguero, Griezmann na Dybala wanaziwinda rekodi hizi ulaya.

Usiku wa michuano ya UEFA Champions League unarejea tena leo usiku na kesho jumatano, katika kukamilisha ratiba ya raundi ya 16 bora na kuamua ni timu zipi zitaungana na Real Madrid, Benfica, PSG na Wolfsburg katika hatua ya robo fainali ya UCL. 
 
Je Lionel Messi atafanikiwa kuifunga Arsenal na kuweka rekodi mpya ya magoli tangu alipoanza kucheza soka la ushindani? Antoine Griezmann atafanikiwa kuifungia Atletico goli la 5 mfululizo? Je Paulo Dybala ataweza kuikoa Juve? 

  Je Griezmann ataifungia Atletico goli 5 mfululizo?
“Nacheza nikiwa na uhuru mkubwa sana, matumaini yangu nitaendelea kucheza kwa mafanikio hivi,” alisema mshambuliaji huyo wa AtleticoMadrid, ambaye yupo on fire akifunga katika mechi 4 mfululizo za La Liga zilizopita tangu Madrid walipotoka sare ya 0-0 n PSV katika mchezo wa kwanza wa 16 bora – Je Atafanikiwa kufunga goli la 5 mfululizo katika mechi 5 mfululizo. 
Rekodi ya PSV kushinda mechi 10 mfululizo katika ligi yao ya Eredivisie iliisha wikiendi iliyopita kwa sare ya 1-1 dhidi ya Heerenven, golikipa Jeroen Zoet akiruhusu wavu wake kuguswa baada ya dakika 603 katika mashindano yote. 
Atlético v PSV, Leo Jumanne.
  Dynamo Kyiv 1-3 Man.City

Agüero na rekodi mpya Man City 
Baada ya kusumbuliwa na Norwich City wikiendi iliyopita, Sergio Aguero akiwa na kikosi cha City atakutana na Dynamo Kiev leo akiwa anaifukuzia rekodi ya kuingia katika 10 bora ya ufungaji katika histori ya Man City.
Aguero amebakiza magoli mawili kumfikia anayeshika nafasi ya 10 kwenye listi hiyo Frank Roberts, huku Billy Gillespie na Fred Tilson wakishika nafasi ya 9&8 kwa kufunga magoli 132 kila mmoja. “Itakuwa kitu kikubwa kuingia katika listi hiyo,” alisema Aguero, ambaye aliiongoza City kushinda 1-3 katika mechi ya kwanza ugenini. 
Manchester City v Dynamo Kyiv, leo Jumanne
  Dybala  tumaini La Juve vs Bayern

Baada ya kufunga goli lake la kwanza katika  UEFA Champions League katika sare ya 2-2  dhidi ya Bayern, mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala akafunga goli lingine zuri mno dhidi ya Sassuolo Ijumaa iliyopita – goli lake la 14 katika msimu wa Serie A. “Hakuna ambaye ameonyesha uwezo wa kufunga na kuchezea mpira akiwa na miaka 22 kama yeye kwenye Serie A,” kocha wa zamani wa Juve Fabio Capello alikiambia Gazzetta dello Sport. “Tayari ameshaonyesha uwezo ndani ya Italy, sasa anahitaji kuonyesha katika michuano ya ulaya.” – Je ataweza kuibeba Juve vs Bayern yenye majeruhi wa kumwaga? Jumatano hii tutapata majibu kutoka Allianz Arena.
  Lionel Messi: Barcelona v Arsenal

Messi mwenye njaa 
Lionel Messi ameshafunga magoli 23 katika mechi 18 ndani ya mwaka huu pekee, na anahitaji kufunga magoli mengine matatu kutimiza magoli 500 (klabu na timu ya taifa). Ingawa alikosa penati katika mechi ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Getafe, alifuta makosa kwa free kick safi. Kiwango chake ni moja ya vitu vinavyowapa Gunners mawazo sana kuelekea kwenye mchezo wa marudiano @CampNou. “Kuvuka ni asilimia 95 kwao na 5 kwetu,” alisema kocha Arsene Wenger ambaye yupo katika hatihati ya kumaliza msimu bila kombe lolote baada ya kutolewa kwenye FA Cup wikiendi iliyopita.  
Barcelona v Arsenal

chanzo>shafiiaduada
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment