NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Usafirishaji Haramu wa Madini Udhibitiwe-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kudhibiti usafirishaji haramu wa madini ya bati, akieleza kuwa yuko mwanamke ambaye si rais wa Tanzania anayesafirisha kinyume cha utaratibu.

Alitaka kujua hatua zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo na kumhoji Mkuu wa Wilaya, Benedict Lenga endapo anafahamu watu wanaosindikiza wezi hao wa madini.

“Madini ni tija, lazima tujue yanasafirishwa kwa kigezo kipi.Tunajua wakati mwingine tunasindikiza watu wanaoiba madini yetu,” alisema Majaliwa na kuhoji endapo Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ndiye anayesindikiza. Hata hivyo, alijibiwa kuwa hahusiki.

Aidha, alimtaka Lenga na watu wake waimarishe ulinzi ili biashara hiyo ya madini idhibitiwe. Majaliwa alikuwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, John Mongella, alipowasili hapa jana kuanza ziara ya siku nne.
 
chanzo>mpekuzi
 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment