VIDEO BAYERN YATINGA ROBO FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE KWA STYLE YA AINA YAKE
Bayern Munich imepambana kutoka nyuma kwa goli 2-0 hadi kuichapa Juventus kwenye dakika za nyongeza na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya Champions League.
Timu hizo zilitoka sare ya kufunga kwa bao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza, Paul Pogba na Juan Cuadrado wakaifungia Juve na kuiweka mbele kwa bao 2-0 dhidi ya Bayern kwenye mchezo wa jana usiku.
Robert Lewandowski alipiga bao kwa kichwa na kufufua matumaini ya Bayern kubadili matokeo kabla ya Juve kumruhusu Thomas Muller kusawazisha katika dakika ya mwisho na kuufanya mchezo kuwa sare ya magoli 2-2 na kulazimisha timu hizo kwenda kwenye dakika za nyongeza.
Bayern wakafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa style ya aina yake baada ya Thiago na Kingsley Coman kuifungia timu yao mabao mawili katika muda wa nyongeza. Mchezo huo ukamalizika kwa Bayern kuichapa Juve magoli 4-2 na kufanya jumla ya magoli yote ya michezo miwili kuwa Bayern 6-4 Juve.
Juve ambao walitawala mchezo kwa asilimia nyingi za muda wa kawaida walichanganywa na goli la kusawazisha la dakika za lala salama la Muller pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Guardiola ya kuwaingiza Coman na Thiago ambao waliamua mchezo.
Mbali na kupoteza mchezo huo, kinachowaumiza zaidi Juve ni goli lilifungwa na Coman mchezaji wao kinda ambaye yupo Bayern kwa mkopo wa muda mrefu.
Kijana huyo wa kifaransa mwenye miaka 19, ali-assist magoli matatu wakati Bayern inashinda bao 5-0 dhidi ya Werder Bremen kwenye mchezo wao wa ligi weekend iliyopita na alikuwa kwenye kiwango bora baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Xabi Alonso.
Angalia video ya magoli yote Juventus 2-4 Bayern Munich
0 comments:
Post a Comment