Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema
jumla ya wafanyakazi 202 katika halmashauri 14 katika mikoa ya Singida
na Dodoma waligundulika kuwa hewa na kulipwa mishahara kila mwezi.
Rais ameyasema hayo alipokuwa akiwakumbusha wakuu wa kikoa wapya ambao amewaapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam.
''Kwa
mikoa miwili tuu wafanyakazi hao 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye
data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine
likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha
ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi''.Amesema Rais Magufuli
Kwa
msingi huo kwa halmashauri 180 nchini ina maana kwa mahesabu ya haraka
haraka kuna wafanyakazi 2000 na zaidi wanalipwa mishahara hewa.
Hivyo
Rais Dkt Magufuli ametoa agizo kwa wakurugenzi wa taasisi za serikali
kuanzia leo ndani ya siku 15 kuhakikisha wanapitia majina ya waajiriwa
wote wa serikali na kuondoa majina ya ambao wanalipwa bila kufanya kazi.
==>Tazama Video hii Kumsikiliza Rais Magufuli Akiongea
==>Tazama Video hii Kumsikiliza Rais Magufuli Akiongea
0 comments:
Post a Comment