Mkuu
wa wilaya ya Singida, Saidi Amanzi amewahimiza wakazi wilayani humo
kufuga kuku wa kienyeji kibiashara ili waweze kupata kipato
kitakachowatoa kwenye lindi la umaskini.
Mkuu
huyo wa wilaya, ametoa wito huo juzi wakati akizungumza kwenye zoezi la
kugawa msaada wa fedha za mpango wa TASAF 111 kwa ajili ya kunusuru
kaya maskini kata ya Ilongero, ambapo zaidi ya shilingi Milioni 13.4
zilitolewa.
Amanzi alisema sio jambo la ufahari mtu mwenye afya njema na ambaye hana ulemavu wa aina yoyote kuendelea kuitwa maskini.
“Niwasihi
sana ndugu zangu kataeni kuitwa maskini.Nawahakikishia mtaondokana na
sifa hiyo mbaya iwapo tu,mtalichukia jina hilo na kujikita kwenye
shughuli halali za kuwaongezea kipato, ikwemo ufugaji wa kuku wa
kienyeji na wale wa kisasa,” alifafanua.
Aidha,
Amanzi amezitaka kaya zinazopata msaada wa fedha za kugharamia masomo
ya watoto wao zihakikishe watoto wao wanasoma kwa bidii ili siku za
usoni waweze kuzikomboa kaya hizo kiuchumi.
“Kwa
upande wenu ninyi mnaoratibu mpango huu wa TASAF,hakikisheni walengwa
kwa maana watu wasiokuwa na uwezo ndio wanaonufaika na sio vingenevyo,”
alisema.
Awali
mratibu wa TASAF mkoani hapa, Patrick Kasango alisema hadi sasa TASAF
111 imetoa msaada wa jumla ya shilingi Bilioni 14.1 kunusuru kaya
maskini 41,321 katika vijiji 280 vya halmashauri sita.
Kasango
alisema baadhi ya kaya hizo, zimetumia misaada hiyo kwa ajili ya
kuanzisha shughuli za kiuchumi ikiwemo ufugaji wa kuku,bata na mbuzi.
Na Nathaniel Limu, Singida
Mratibu
TASAF mkoa wa Singida Patrick Kasango,akizungumza kwenye hafla ya
kugawa fedha za mpango wa TASAF 111 kunusuru kaya maskini katika tarafa
ya Ilongero juzi. Wa kwanza kushoto (walioketi) mkuu wa wilaya ya
Singida Saidi Amanzi na katikati ni mwenyekiti wa kijiji cha Ilongero.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Saidi Amanzi,akizungumza kwenye hafla ya kugawa
fedha za mpango wa TASAF 111 katika tarafa ya Ilongero juzi.Amanzi
amewataka wakazi wa wilaya hiyo,kuanzisha ufugaji wa kibiashara wa kuku
wa kienyeji,ili waweze kujipatia kipato na hivyo kuondokana na
umaskini.Wa kwanza kulia (walioketi) ni mratibu wa TASAF mkoa wa
Singida, Patrick Kasango na katikati ni mwenyekiti wa kijiji cha
Ilongero.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Saidi Amanzi,akigawa fedha za TASAF mpango wa 111 kunusuru kaya maskini katika kata ya Ilongero.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Saidi Amanzi (aliyenyoosha mikono), akisisitiza
jambo kuhusiana na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mwahango kata ya
Ilongero inayojengwa na TASAF 111. (Picha na Nathanile Limu)
0 comments:
Post a Comment