WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi maofisa watano wa Idara ya Misitu
mkoani Rukwa kwa kushindwa kusimamia vema na kudhibiti uvunaji haramu wa
magogo.
Waliosimamishwa ni Kaimu Meneja wa
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Nyanda za Juu Kusini, Bruno Mallya na
Mshauri wa Maliasili Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa, Nicholas Mchome
kupisha uchunguzi.
Wengine
waliosimamishwa kazi ni Ofisa Misitu wa TFS, Helman Ndanzi na Ofisa
Misitu daraja la II, Geofrey Mwasomola wote kutoka wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa. Mwingine ni Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)
Sumbawanga na Kalambo, Martin Hamis.
Profesa Maghembe alisema amelazimika
kuwasimamisha kazi maofisa hao kwa kushindwa kusimamia vema na kudhibiti
uvunaji haramu wa magogo aina ya mkurungu na kusababisha uharibifu
mkubwa katika Msitu wa Kalambo.
Pia wanadaiwa kuruhusu makundi makubwa
ya mifugo kuchungwa katika msitu huo bila kuchukua hatua stahiki kwa
wavamizi. Aliwaagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa TFS, kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa.
“Wewe Kaimu Meneja wa TFS
Kanda (Mallya ) kazi basi mpaka uchunguzi wote utakapokamilika pia Ofisa
Misitu wa Mkoa wa Rukwa (Mchome) …tutaleta maofisa wengine wanaoweza
kulinda rasilimali za Serikali kwa kuwa nyie mmeshindwa na hamna uchungu
wa rasilimali za nchi hii,” alisema Maghembe.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WAZIRI MAGHEMBE AWATUMBUA VIGOGO WA MISITU RUKWA
Reviewed by Newspointtz
on
10:56:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment