MICHEZO saba ya Ligi Kuu ya Bara,
inatarajiwa kuchezwa katikati ya wiki hii, huku leo kukichezwa mchezo
mmoja wa Yanga inayotaka kurejea kileleni dhidi ya Africans Sports
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Licha ya mchezo huo michezo mingine sita itachezwa kesho na keshokutwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Akizungumza na simba makini leo asubuhi,
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema leo
jioni watakuwa wamesharejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Alisema wanafahamu ugumu wa ligi ulipofikia hivi sasa, hivyo hawawezi kukubali kupoteza pointi kirahisi.
“Leo jioni tutarudi katika nafasi yetu,
hao walioko juu (Simba) wameisj=hika hiyo nafasi kwa muda maalum tu,
lakini mpaka kufikia jioni tutakuwa kileleni kwetu.
“Ligi ya msimu huu imekuwa ngtumu na
kila mchezo unahitaji kushinda ili kuongeza wigo wa pointi na timu
zilizo nyuma yako” alisema Muro.
Hata hivyo nahodha wa Africans Sports, Mendy James alisema wanafahamu jinsi ya kucheza na Yanga na kupatra matokeo.
James, alisema wanaingia katika mchezo
huo wakiwa katika malengo mawili tofauti kwa wao kutaka kujinasua mkiani
na Yanga kutaka kwenda kileleni.
Mchezo wa kwanza wa timu hiyo uliofanyika Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani, ulimalizika kwa Yanga kupata ushindi wa bao 1-0.
Ikitokea Yanga wameshinda mchezo huo
watakuwa wamefikisha pointi 50 na kuishusha Simba kileleni ambayo
watabaki na pointi zao 48.
Licha ya mchezo huo wa leo kesho
Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya, huku Coastal Union wakicheza na ndugu zao maafande
wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Majimaji
katika Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, huku JKT Ruvu
wakiwakaribisha Toto African katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoa
wa Pwani.
Alhamisi Simba SC watawakaribisha Ndanda
FC kutoka Mtwara katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku
wagonga nyundo wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City wakiwakaribisha Stand
United chama la wana katika uwanja wa Sokoine.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
YANGA SC KUREJEA KILELENI LEO?
Reviewed by Newspointtz
on
13:55:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment