NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Alichokisema Dogo Richie kuhusu muziki na Baraka Da Prince

Moja kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye muziki mzuri ni pamoja na Dogo Richie a.k.a “Richie Ree” ingawa bado kunawatu hawaja mtambua vizuri muziki wake. Baada ya kuisikiliza na kuitazama video ya wimbo wake mpya “Yoyoba” na kupitia nyimbo zake kadhaa  na haya ndiyo maisha yake ya Muziki aliyofunguka na kusema.

“Kwa majina naitwa Francis Kazungu Kalama Jina la sanaa Dogo Richie a.ka Richie Ree, Baba yangu ni Mkenya Mama yangu ni Mtanzania mimi ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto 6, nilianza muziki 2013 Studio yangu ya kwanza kuingia ilikuwa ni ‘Jungle Masters’ chini ya Producer ‘Emmy D’ ambaye ndiye Producer wangu hadi sasa.

Hadi kufikia sasa nina jumla ya nyimbo 4 na Collabo moja Naona raha, Sina raha, Yoyobah, Hayana Mjuzi & So nice ft. Sam Wa Ukweli. ‘Naona raha’ ni moja kati nyimbo zilizo nitambulisha vizuri, 

Muziki katika maisha yangu ndio kila kitu no muziki hakuna kinachoweza kwenda ingawa kupitia muziki nimeweza kuanzisha biashara zangu ndogo ndogo ambazo pindi napo kuwa sina Show zinakuwa zinanisaidia kuendesha maisha.

Baraka Da Prince ni msanii ninaye mfagilia sana Tanzania, coz anamuziki mzuri, Changamoto kwenye muziki zipo ila kikubwa ambacho nakiona kwangu ni ‘Marketing’ ya muziki wangu ili uweze kufika mbali zaidi, coz malengo yangu ni makubwa yaani ni kufika level za kimataifa.

Mwisho nimshuru mwenyezi Mungu, Fans wangu na wadau wote wanao endelea kunipa support kwenye Muziki maana wao ndio maisha yangu Thanks”
Waweza kuona video hiyo hapa chini:
 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment