BARCA yanusa nusu fainali UEFA
Luis Suarez amepiga bao mbili Barcelona ikitoka nyuma na kuichapa Atletico Madrid 2-1 ikiwa na watu 10 uwanjani kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League.
Atletico ilifanikiwa kupata goli muhimu la ugenini wakati Fernando Torres alipofanya kazi ya ziada kupachika bao hilo kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Lakini game ilibadilika muda mfupi baada ya Torres kutolewa nje kabla ya half-time baada ya kuonesha kadi mbili za njano ndani ya dakika saba.
Brca ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo walichachamaa tangu kuanza kwa kipindi cha pili ambapo Suarez alifanikiwa kusawazisha goli kabla ya kupachika bao la ushindi kwa kichwa kikali.
Hatahivyo, ilikuwa ni bahati kwa Suarez kumaliza mchezo huo bila kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kufanya makosa kadhaa ambayo si ya kiungwana kwenye mchezo wa soka ikiwa ni pamoja na ‘kumpiga kiatu’ kwa makusudi beki wa kulia wa Atletico Juanfran.
Timu hizo zinasubiri game ya marudiano kwenye dimba la Vicente Calderon siku ya Jumatano ya juma lijalo.
Torres kutoka kuwa shujaa hadi kuharibu
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea alipachika bao la ugenini akiunganisha pande la kiungo mkabaji Koke huku glikipa wa Barca Marc-Andre ter Stegen akishindwa kuuzuia mpra ambao ulipita katikati ya miguu yake ‘tobo’.
Torres alioneshwa kadi ya njano ya kwanza kwa kumchezea madhambi Neymar kisha baadaye akaoneshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Sergio Busquets na kujikuta akitupwa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu.
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone alishangazwa na maamuzi ya referee wa kijerumani Felix Brych ambaye pia aliwahi kutoa nje kwa kadi nyekundu Arda Turan kwenye mchezo wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Real Madrid msimu uliopita
Kocha huyo kutoka Argentina anaweza akaamini timu yake haikutendewa haki kutokana na tukio la Suarez kumpiga ‘buti’ Juanfran wakati akiwa hana mpira lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa dhidi yake.
Mbinu za Atletico zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa
Wakiwa pungufu kwa mchezaji mmoja, Atletico bado waliendelea kuziba mianya na kupunguza kasi ya Barcelona waliokuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani na kufanikiwa kutofungwa idadi kubwa ya magoli.
Barcelona walishindwa kuhimili usumbufu wa Atleico mwanzo mwa kipindi cha kwanza na kujikuta wakishambuliwa kila mara.
Atletico walitaka kuwachanganya Barca kwa kuwazuia kucheza soka lao la pasi nyingi na walifaniwa baada ya Torres kupachika kambani bao la kuongoza.
0 comments:
Post a Comment