NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Bulembo akerwa na mmomonyoko wa maadili

Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakipiga picha pamoja na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Abdala Bulembo (wa sita kutoka kushoto mtari wa kwanza)katika maadhimisho ya jumuia hiyo 9/4 kila mwaka kitaifa yalifanyika Mkoani Morogoro.Picha na Timotheo Lupembe




Na.Timotheo Lupembe-Morogoro

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mh Abdala Bulembo, amekemea tabia ya Wazazi na walezi wa watoto Nchini kubaka na kuwalaiti watoto wa kufikia hali inayovunja maadili ya kitanzania.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mh Abdala Bulembo katika maadhimisho ya miaka 61 ya jumuia hiyo kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro

“Nikiwa kama mzazi nachukiza na hii tabia ambayo inashamiri katika sehemu mbalimbali za nchi kiasi ambacho inavunja mila na tamaduni za watanzania na kuomba ichukuliwe hatua ili kukomesha tabia hii kwa baadhi ya wazazi” alisema Bulembo


Aidha Mh Bulembo alitumia siku ya maadhimish ya siku ya Wazazi kuunga mkono jitihada na hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ya awanu ya tano ya Mh Dr John Pombe Magufuli.

“Natumia fursa hii kwa niaba ya Wazazi wote kumpongeza mhesimiwa Rais Dr Magufuli katika jitihada zake za kuhakikisha miiko na taratibu za kazi zinafuatwa  na kufanya nchi yetu iweze kusonga mbele”aliongeza Bulembo

Siku ya Jumuia ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM inaazimishwa kila ifikapo tarehe 9 mwezi wa 4 kila mwaka
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment