Goli la mapema la Arturo Vidal limeipa Bayern Munic ushindi dhidi ya Benfica kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Kiungo huyo aliunganisha kwa kichwa krosi ya Juan Bernat ikiwa ni shambulizi la kwanza kufanywa na Bayern kwenye game hiyo.
Bayern ilishindwa kuipangua tena ngome ya ulinzi ya Benfica na kufunga magoli zaidi kwa faida ya kucheza nyumbani.
Benfica ilishindwa kulazimisha sare ya bao 1-1 baada ya shuti kali la Jonas kuzuiwa na Javi Martinez.
Bayern ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali kila mwaka tangu 2012, itatakiwa kujiimarisha kabla ya mchezo wa marudiano Jumatano ya wiki ijayo mchezo utakaopigwa Ureno.
Benfica watapindua matokeo kwenye mechi ya marudiano?
Ulikuwa ni mchezo wa pili kupoteza kwa Benfica kati ya michezo yao 21 huku inkiwa ni miongoni mwa timu zenye viwango bora barani Ulaya kwa sasa.
Mshambuliaji wao wa kibrazil Jonas ameshafunga magoli 32 kwenye mashindano yote msimu huu, lakini alipoteza nafasi mbili za wazi wakati wa mchezo dhidi ya Bayern.
Benfica bado wanaamini Jonas pamoja na mshambuliaji mwenzake Kostas Mitroglou mwenye magoli 21 wanaweza wakafanya kwenye mchezo wa marudiano wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
0 comments:
Post a Comment