Chicharito
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United anayekipiga kwa sasa katika klabu ya Bayer Leverkussen ya Ujerumani, Javier Hernandez “Chicharito” amefunguka kuwa kabla ya kujiunga Leverkusen alikuwa akihitajika na vilabu vikubwa vya Italia lakini alivipiga chini.

Akizungumza na Gazzetta dello Sport, Hernandez alisema alihitajika na vilabu vya Italia lakini aalichagua Leverkusen sababu aliona wana nafasi nzuri ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Juventus, Inter Milan, AC Milan, Lazio na Roma walijaribu kunisajili katika kipindi cha joto,” alisema Chicharito na kuongeza.

“Nilichagua Leverkusen sababu ya Ligi ya Mabiingwa Ulaya na walinifanya nihisi nahitajika. Walinishawishi na ninatakiwa niwasaidie na hilo litanifanya nitabasamu kila wakati … nina mkataba nao mpaka 2018 na nina kila kitu ninachohitaji pale”