Kiasi
cha Sh milioni 473 kinahitajika ili kulipa fidia ya ziada kwa wananchi
wanaopaswa kuondoka ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma.
Hatua hiyo ilikuja baada ya wananchi kuweka pingamizi mahakamani wakidai malipo fidia waliyolipwa awali ni madogo.
Akitoa
taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) mkoani Kigoma,
Mohammed Suleiman alisema hatua ya kuongeza fedha hizo za ziada inalenga
kumaliza malalamiko ya fidia yanayoukabili mradi huo.
Suleiman
alisema katika mpango huo wanatarajia kutoa nyongeza ya Sh 500,000 kwa
kila mwananchi anayetakiwa kupisha upanuzi wa uwanja huo, hatua
itakayowafanya wananchi waondoe kesi mahakamani na hivyo ujenzi kuanza.
Alisema
kiasi cha Sh milioni 650 zilishalipwa kama fidia kwa nyumba, viwanja,
mashamba na mazao na kiasi cha Sh milioni 645 zililipwa kama fidia kwa
makaburi 2,786.
Meneja
huyo wa TAA alisema kuwa utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa njia ya
kurukia ndege utawezesha njia hiyo kufikia mita 3,100 na hivyo kuwezesha
ndege kubwa ikiwemo Boing 737 kutua na kwamba kwa sasa awamu ya kwanza
ya mradi huo imewezesha njia hiyo kufikia mita 1800.
Alisema
mradi wa jengo la kisasa la abiria na mnara wa kuongozea ndege
unatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu na kwamba michakato ya
utekelezaji wa mradi huo inaendelea kwa hatua mbalimbali.
Akizungumzia
taarifa hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, alieleza
kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma
Ujiji kupenda kuzuia miradi ya maendeleo mahakamani kwa kulalamikia
fidia.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment