NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Gerald Hando na Paul James aka PJ Wanaelekea EFM Baada ya Kuachwa na Clouds FM

Kuna tetesi kuwa Gerald Hando na Paul James aka PJ wanaelekea EFM baada ya kuacha kazi Clouds FM walikojizolea umaarufu kwenye kipindi cha Power Breakfast.
 
Hando, PJ na Barbara waliziba pengo la Masoud Kipanya na Fina Mango waliokuwa watangazaji wa kipindi hicho chenye wasikilizaji wengi kwa miaka kibao. Jana, kipindi hicho kiliwapa surprise wasikilizaji wake kwa kuwaleta tena Fina na Masoud, na kwa waliosikiliza kipindi hicho, watakubali kuwa mambo yalipendeza.
 
Swali ni kwamba wawili hao ndiyo wamerejea tena Clouds FM? Fina alikuwa na kipindi chake Magic FM kiitwacho Makutano, je kimekufa? Tunafahamu kuwa Masoud yuko available kwa sasa hivyo uwezekano wa yeye kurejea kwenye redio yake ya zamani ni mkubwa.
 
Wengine wanaamini kuwa wawili hao walifanya kipindi hicho tu na hawatarejea tena. Lakini kama wakirejea, basi ushindani kwenye vipindi vya asubuhi hasa ukizingatia kuwa PJ na Hando wataenda EFM, utakuwa mkubwa.
chanzo>www.udakuspecially.com



Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment