Baada ya tukio lililotokea kwenye mchezo
wa Simba na Toto African la golikipa wa Simba Vicent Agban kumpiga beki
wa kulia wa timu hiyo Hassan Ramadhani Kessy mambo yamebadilika kwenye
timu hiyo na huenda yakawa makubwa zaidi kutokana na hali ilivyosasa.
Uongozi wa klabu ya Simba umemwambia
beki wake wa kulia Hassan Ramadhani ‘Kessy’ anaweza kuondoka kwenye timu
yao baada ya mchezaji huyo kusema hatoendelea kuichezea timu hiyo tena
kufuatia kupigwa na kipa Mu-Ivory Coast Vicent Agban baada ya mchezaji
huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi ya Vodacom
dhidi ya Toto Africans.
Mkataba wa beki huyo kuihudumia Simba
umebakiza mwezi mmoja na kwa hali ilivyo kunauwezekano mkubwa ataondoka
kutafuta timu nyingine ya kucheza zikiwemo Yanga au Azam.
Msemaji wa Simba Hajji Manara, amesema
mchezaji huyo anaweza kwenda kwasababu wamechoshwa na mambo yake na
Simba haimtegemei yeye hivyo anaweza kuondoka na timu yao bado ikafanya
vizuri kwenye mechi za ligi.
“Simba
siyo Baba yake wala Mama yake amezaliwa ameikuta na kuna wachezaji wengi
mahiri pia wameiacha kwahiyo kama kweli ametamka maneno hayo anaweza
kuondoka na wala hatuta tetereka kwasababu hivi sasa yupo mbona timu
inashika nafasi ya pili na tumefungwa nyumbani na timu ndogo ya Toto,”amesema Manara.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Hassan kessy njia yeupe kuondoka Msimbazi
Reviewed by Newspointtz
on
06:49:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment