Cristiano Ronaldo ameushangaza ulimwengu kwa mara nyingine tena baada ya kusukuma kambani goli tatu huku Real Madrid ikipindua matokeo ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa bao 2-0 dhidi ya Wolfsburg na kutinga nusu fainali ya UEFA Champions League.
Wolfsburg walitua kwenye mji mkuu wa Hispania wakiwa mbele kwa hazina ya magoli 2-0 mbele ya Madrid waliyofunga kwenye uwanja wao wa nyumbani, lakini walijikuta wakisawazishiwa magoli hayo ndani ya sekunde 86 za kipindi cha kwanza.
Mreno huyo aliiandika timu yake bao la kwanza akiwa umbali wa mita sita kutoka lanoni kabla ya kupachika bao la kusawazisha kwa kichwa murua na kufanya matokeo ya jumla (aggregate) kuwa 2-2.
Ronaldo alikamilisha hat-trick goal kwa goli la mpira wa adhabu ndogo goli ambalo lilimaliza ndoto za Wolfsburg kusonga mbele kwenye michuano hiyo mikubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.
Goli la tatu la Ronaldo limeweka hai ndoto za mabingwa hao mara 10 wa ligi ya Mabingwa Ulaya na kufufua matumaini ya kutwaa chochote msimu huu baada ya kikosi hicho ambacho kipo chini ya Zinedine Zidane awali kuonekana kama tayari kimemaliza msimu baada ya kuchapwa ugenini juma lililopita.
Kutana natakwimu za Ronaldo na Madrid ndani ya UEFA Champions League
- Ronaldo amefunga magoli 34 (na ana-assist nane) kwenye mechi 36 za Champions League hatua ya mtoano akiwa Real Madrid.
- Ronaldo amefunga magoli 62 kwenye mechi tofauti za Champions League; zaidi ya mchezaji yeyote (anafuatiwa na Raul mwenye magoli 56)
- Nyota huyo wa Ureno amesha kwamisha mpira nyavuni mara 16 kwenye mashindano ya Champions League msimu huu.
- Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kati ya mara 16 timu kupoteza mchezo wa ugenini kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Champions League kisha kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano (Barcelona vs AC Milan 2013 na Man United vs Olympiacos 2014)
- Madrid ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu kufungwa bao kwenye uwanja wake wa nyumani kwenye michuano ya Champions League msimu huu.
0 comments:
Post a Comment