Hadi
kufikia tarehe 18/04/2016 Mkoa wa Iringa umefanya zoezi la uhakiki wa
watumishi kwa awamu mbili awamu ya kwanza, uhakiki ulifanyika kuanzia
tarehe 16/03/2016 na kukamilika tarehe 26/03/2016 ambapo jumla ya
watumishi 15walibainika kuwa ni watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa
ambao waliisababishia Serikali hasara ya Shilingi 81,921,725.08.
Katika
uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haikuwahakiki
watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo imekamilisha
uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili
kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa,
niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na
Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili.
Nimepokea
taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi
hewa kumi na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao
wameisababishia Serikali hasara ya shilingi 155,205,681/=
Watumishi hao wapo katika mchanganuo ufuatao:
Uhakiki
uliofanywa na Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
umebainisha kuwapo kwa watumishi tisa (9) ambao ni watoro na mtumishi
mmoja ambaye aliomba likizo bila malipo na kwenda kufundisha mahala
pengine lakini akaendelea kulipwa mpaka kufikisha kiasi cha Tsh. 25,
831,000/= lakini baada ya kufanya ufuatiliaji amerejesha kiasi cha Tsh.
18,604,679/= Mtumishu huyu ni mwalimu anaitwa Dinner J. Kissamo alikuwa
mwalimu Manispaa ya Iringa.
Aidha,
Uhakiki pia ulibaini mwalimu mmoja (Ifunda) alikuwa na Check 2 na zote
alikuwa analipwa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Uchunguzi zaidi
unaendelea kufanyika.
Mtumishi
Mwingine ni Khalid M. Meza Afisa kilimo Kilolo ni mtoro wa muda mrefu
mkurugenzi tayari ameshamfungulia mashtaka. Hii ni mifano tu ya
watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuendelea kujiridhisha na kuondolewa kabisa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa, nimechukua hatua zifuatazo;
1.
Nimewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa, zoezi la uhakiki
watumishi linakuwa endelevu na hatua zinachukuliwa ili kuwaondoa
watumishi hewa wote
0 comments:
Post a Comment