Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi amewaasa Wakuu wa
Mashirika na Taasisi za Umma kuzingatia Maadili ya Viongozi wa Umma
katika kutekeleza makujumu yao.
Katibu Mkuu alisema hayo jana
jijini Dar es salaam wakati wa akifungua mafunzo ya viongozi hao
yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ili kuhakikisha wanaendana Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli.
“Maadili
yana umuhimu wake mkubwa katika utawala wa maendeleo ya nchi, kupitia
maadili mema wananchi wanajenga imani na viongozi pamoja na Serikali yao
kwa ujumla” alisema Balozi Mhandisi Kijazi.
Ili
kuhakikisha mafunzo yanakuwa yenye tija, Balozi Mhandisi Kijazi
amewasisitiza viongozi hao kutumia muda vizuri na kujikumbusha na
kujifunza maadili hayo kwa manufaa ya mashirika na taasisi zao pamoja na
taifa kwa ujumla.
Balozi
Mhandisi Kijazi alitaja umuhimu wa maadili katika jamii na kusema kuwa
yanasaidia kusimamia rasilimali za umma na kuzitumia kwa maslahi ya
wote, kuongeza tija na thamani ya huduma, zinazotolewa na Serikali,
kudhibiti mianya ya ukiukwaji wa maadili na vitendo vya rushwa, kujenga
ujasiri wa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma.
Maadili
pia yanasaidia wananchi, viongozi na Watumishi wa Umma kutoa mchango wa
haraka katika kutekeleza maendeleo ya nchi, kuepuka utata wa maamuzi ya
migongano ya kimaslahi, kuwavutia wawekezaji, kujenga na kudumisha
amani na utulivu pamoja na kuondoa na kukomesha ubinafsi kwa viongozi.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi alisema
kuwa ukiukwaji wa maadili unaathari hasi kwa taifa ambapo alizitaja
baadhi ya athari hizo kuwa ni rasilimali za nchi kunufaisha wachache,
wananchi kukosa haki zao za msingi kutokana na rushwa na upendeleo,
viongozi wa umma kujilimbikizia mali isivyostahili bila kujali hali za
wananchi wanaowaongoza, kupungua kasi ya uwekezaji pamoja na kudhohofika
kwa uchumi wa nchi.
Madhara
mengine ya kutojali maadili ni wananchi kukosa imani na Serikali yao,
kuchochea vurugu pamoja na wananchi kutotii sheria za nchi na hivyo
kuhatarisha usalama, amani na utulivu wa nchi.
Kwa
upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Jaji Mstaafu Salome Kaganda alipokuwa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi alisema
kuwa misingi ya maadili na maadili yanalenga katika kuzuia mgongano wa
maslahi, upendeleo, matumizi mabaya ya rasilimali za umma na taarifa za
ofisi na mwenendo usiofaa kwa viongozi wa umma ili kuimarisha na
kuendeleza dhana za uadilifu, uwajibikaji na uwazi ambazo ni sifa
muhimu za kiongozi.
Ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, Jaji Mstaafu Kaganda alisema
kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu
wa watumishi ambapo kuna zaidi ya viongozi 15,000 huku Sekretarieti ina
wafanyakazi 200 nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment