NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Makamu wa Urais Mh.Samia Suluhu aendelea na ziara mkoani Morogoro


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro leo April 17,2016, wakati alipowasili Hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolea kwa Jamii katika Hospitali hiyo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. kulia Daktari Mfawizi wa Hospitali hiyp Dr. Rita Lyamuya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimfariji Bibi Fausta Andreas na Mtoto wake Vayalet Michael (2)
aliyelazwa katika Hospitali ya rufaa Mkoa Morogoro kwa matibabu wakati
alipotembelea Hospitali hiyo leo April 17.2016 kwa ajili ya kuangalia
utendaji na utoaji huduma kwa Jamii. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro
kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimfariji Mtoto Anisha Juma (2) mkazi wa Morogoro mjini aliyelazwa
katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu leo April
17.2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuangalia
utendaji kazi na utoaji huduma kwa Jamii.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mafundi Seremala cha (Kimasemo) kiliopo Sabasaba Mkoani Morogoro, wakati alipotembelea Kiwanda hicho leo April 17.2016 kwa ajili ya kukagua kazi zinazofanywa na kikundi hicho ambapo ameahidi kuchangia jumla ya Tshs 10 milioni kwa ajili ya kuendeleza utendaji wa kiwanda hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Korogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment