NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Mashabiki wa AL AHLY wavamia Taifa ,wapiga Waandishi

Askari wa jeshi la polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi mashabiki wa Al Ahly baada ya kufanya fujo kwenye uwanja wa taifa wakati timu yao ikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kupambana na YangaAskari wa jeshi la polisi wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi mashabiki wa Al Ahly baada ya kufanya fujo kwenye uwanja wa taifa wakati timu yao ikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kupambana na Yanga

Tukio hilo limetokea wakati Al Ahly ilikuwa ikifanya mazoezi ambapo mara baada ya kukuta geti limefungwa mashabiki hao wasiopungua 45 waliamua kuruka ukuta na kumkuta mwandishi wa Azam Media Gedion Mkude na kuanza kumshambulia wakimzuia kuwachukua kwa kamera yake.

Baada ya tukio hilo Gedion alitoa taarifa kwa Meneja wa Uwanja ambaye naye alimpigia simu mkuu wa kituo cha Chang’ombe ambaye alifika na kuwachukua mashabiki hao ambao hata walipokamatwa hawakuonekana kujali chochote

Mpaka Shaffihdauda inaondoka katika kituo cha Chang’ombe baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakiendelea kutoa maelezo juu ya tukio hilo.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment