Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya
jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika
kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League).
TFF
imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF
yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C
baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
Mbao
FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya
kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na
JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo.
Timu
ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za
African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa
Pwani.
Wakati
huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa
Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali
ambazo zimekatwa na kutokana na maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF.
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF itasikiliza rufaa za wafuatao waliokata rufaa
(i) Saleh Mang’ola,
(ii) Yusuph Kitumbo,
(iii) Amos Mwita,
(iv) Fateh Remtullah,
(v) Timu ya JKT Oljoro,
(vi) Timu ya Polisi Tabora.
Aidha Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Jumapili Mei Mosi kupitia taarifa mbalimbali zilizowasiliswa katika kamati hiyo.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook
, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment