Huku tetesi za kujiunga kwake na Manchester United zikiwa zimeshika
hatamu, leo kocha wa kireno Jose Mourinho amefanya mahojiano
yaliyochapishwa na gazeti la Ureno O Jogo.
Kocha
huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid amesisitiza anatarajia
kufundisha wakati wa kiangazi lakini hana uhakika atafundisha timu
gani.
Jose Mourinho amekaririwa akisema kwamba ana ofa kadhaa mezani lakini anataka kwenda sehemu ambayo anahitajika kiukweli.
“Ninakuhakikishia kwamba nitarejea kazini wakati wa kiangazi. Nina ofa nzuri mezani.
“Ni jambo la kufikiria, kisha kufanya maamuzi sahihi na kusaini
mkataba. Wakati wa kiangazi, mwishoni mwa msimu, kila mtu atafahamu
klabu yangu mpya.”
“Kitu cha uhakika, sitkuwa kocha wa Estoril au Paços, kwa sababu wote wana misimu mizuri na hawawezi kubadili kocha.”
“Nitapeleka ujuzi wangu sehemu ambayo nahitajika kwa dhati. Nataka niende sehemu ambayo natakiwa niwepo kiukweli.”
“Nataka kufanya kazi katika klabu ambayo ina majukumu mazito, kwenye
ligi ngumu, ambapo hakuna malengo mepesi. Hayo yananifanya nisiwe na
machaguo mengi.”
Sentensi hii ya mwisho inaonyesha kwa kiasi fulani kwamba Mourinho
anaelekea England kwenye ligi yenye ushindani mgumu – klabu yenye
majukumu mazito ambayo kwa sasa inayumba ni Manchester United. Klabu
nyingine ya ligi nyingine ngumu yenye sifa alizotaja ni Real Madrid.
Wachambuzi wengi wa michezo barani wanaamini Mourinho ataenda Old
Trafford na tangazo lake la ajira litatolewa mwishoni mwa msimu au pale
itakapothibitika kimahesabu kwamba United haitoweza kumaliza katika
nafasi 4 za juu za kufuzu ulaya – Van Gaal atakutana na barua ya
kuvunjiwa mkataba na Mourinho atatangazwa kumrithi kuanzia msimu ujao.
Home / Sports
/ Mourinho azungumzia ajira mpya – viashiria vinaonyesha Old Trafford ndio kituo kipya cha ajira.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment