Watu
wasiofahamika wamelipua kwa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu Ofisi ya
Wakili wa Kujitegemea, Omar Said Shabani, iliyopo Kiembe Samaki
Zanzibar.
Tukio
hilo lilitokea saa 7:00 usiku wa kuamkia jana. Hata hivyo, hakuna mtu
aliyejeruhiwa kutokana na mlipuko huo isipokuwa jengo la ofisi hiyo
limeharibika katika baadhi ya maeneo ikiwamo kuvunjika kwa vioo vya
madirisha.
“Majira
ya saa saba usiku, nilipata taarifa kuwa mlipuko umetokea katika ofisi
yangu na nilipofika nilikuta mipasuko kidogo ya vioo vya nyumba yangu," alisema Wakili Omar.
Omar, ambae pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, alisema gharama za uharibifu wa mali hiyo bado hajazijua.
Aidha, alisema analiachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha
kutokea kwa mlipuko huo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na
uchunguzi ili kubaini aina ya bomu lililotumika.
Alisema taarifa kamili kuhusu mlipuko huo, atautoa baadaye kwa vile polisi wanaedelea na uchunguzi.
Aidha,
Kamanda Mkadam aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu na
kutoa taarifa ya vitendo vyote vinavyoashiria uhalifu.
0 comments:
Post a Comment