MV Malagarasi
Muonekano wa kivuko cha MV. Malagarasi kilichopo katika eneo la Ilagala mkoani Kigoma. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100, magari sita na tani 50 kwa wakati mmoja.
Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), akipata maelezo ya kivuko cha MV. Malagarasi kutoka kwa Msimamizi wa Kivuko hicho kabla ya kukikagua. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani kigoma Eng. Narcis Choma na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe.
Makame Mbarawa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuka katika Kivuko cha MV. Malagarasi mara baada ya kukikagua na kuona namna ya kivuko hicho kinavyofanya kazi.
MV Malagarasi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akioneshwa vifaa vya uokoaji katika kivuko cha MV. Malagarasi.
MV Malagarasi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akijadiliana jambo na mmoja wa abiria wa Kivuko cha MV. Malagarasi.
MV Malagarasi
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa wananchi wa Ilagala, Sunuka, Karago, Herembe, Kapalamsenga, Mgambazi, Lukoma hadi Kashagulu ya namna sahihi ya kutumia kivuko cha MV. Malagarasi, mkoani Kigoma.
Makame Mbarawa - Kigoma
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia), wakati wa mkutano na wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa zao katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Makame Mbarawa - TTCL
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu nchini (TTCL) katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati waliokaa). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura.(Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano).