Mwenyekiti wa kamati ya wanawake kanda ya kati(RAAWU) Bi.
Gaudincie Leo Donati,Jana katika kikao cha tathimini ya chama hicho
kilicho fanyika kwenye viwanja vya bwalo la( JKT) mjini Morogoro
aliwataka wajumbe wa kikao kuthamini jitihada zinazo fanywa na chama
katika kutetea wanachama wake.
"Ukiwa kiongozi unatakiwa utambue majukumu yako, na kazi
yetu kubwa ni kuwatetea wanachama kwetu" Alisema Bi.Gaudiencia Leo
Donati.
Katika kikao hicho cha tathmini mjumbe wa RAAWU tawi la
chuo kikuu cha kilimo(SUA) Bi. Hidaya Ahmadi kwa niaba ya wajumbe
wenzake walimuomba mwenyekiti wa kamati ya wanawake
Bi. Gaudiencia Leo
Donati ambaye anamaliza muda wake, aweze kuwakubalia wajumbe aendelee
kugombea nafasi hiyo na wote kwa pamoja wamuunge mkono.
"Mwenyekiti pamoja umesema hiki ndio kikao chako cha mwisho
ukiwa kama mwenyekiti wa kamati ya wanawake kanda, sisi hapa kwa umoja
wetu yupo tayari kukuchukulia fomu na kujaza uweze kuendelea kutuongoza"
alisisitiza Bi.Hidaya Ahmadi.
Naye katibu wa RAAWU mkoa wa Morogoro, ndugu Baraka Issa
aliwataka wajumbe wajiweke tayari kwa maandalizi ya siku wa wafanyakazi
itakayo fanyika siku tarehe 1 mwezi wa 5 ambayo kimkoa itafanyika
Morogoro na kitaifa itafanyika Dodoma.
" mjiweke tayari kwa maandalizi ya ya mei mosi, na kwa
tathimini hii iwe mwongozi wetu katika shughuli zinazofuata" Aliongezea
ndugu Baraka Issa.
Kikao hicho kilifanyika kufanya tathimini ya kuangalia
namna chama kilivyo adhimisha siku ya wanawake Duniani inayo adhimishwa
kula ifikapo 8/3
0 comments:
Post a Comment