Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 imemkumba mwanadada ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa staa wa Bongo fleva, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema anayeishi Mwanza baada ya kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka miwili.
Hukumu
hiyo imetolewa na Mahakama Kuu ya Mkoani Mwanza ambapo Siwema
amehukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kumtukuna matusi mtu kwa njia
ya mtandao kitu ambacho ni kinyume cha sheria nchi. Siwema alituhumiwa
kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa
jina la Deo.
Akihojiwa
na baadhi vyombo vya habari, mzazi mwenzake na Siwema ambaye ni Nay wa
Mitego alikiri kupokea taarifa hizo za mzazi mwenziye kufungwa huku
akisisitiza kuwa anaangalia uwezekano wa kumsaidia mwanamke huyo.
“Taarifa
nimezipokea ni kweli Mzazi mwenzangu (Siwema) amefungwa na ninakumbuka
nilipoamka tu nikakutana na missed calls za ndugu zake kadhaa ambao
wananifahamu nikahisi kuna kitu maana sio kawaida watu kunipigia mara
kwa mara, kumpigia akaniambia Siwema amehukumiwa miaka miwili jela
sikuamini ikanibidi nimpigie tena ndugu wa karibu naye akanithitibishia
hivyo.
“Kosa
unajua mimi nilishasahau kwamba kitu chochote kichotokea kipindi cha
nyuma kwasababu ni muda kidogo na pia sikuwa naye kwenye mawasiliano ila
niliachoambiwa kuwa amehukumiwa miaka miwili kutoka na kosa lake,
nimejikuta nimekuwa mnyonge nimeingia imani kusikia habari hiyo.
“Napambana
jinsi ninavyoweza kuona namna ninayoweza kumpa msaada kwa njia yoyote
ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa.” alisema Nay.
Nay
wa Mitego aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kwa muda mrefu na
Siwema na kubahatika kuzaa naye mtoto aitwaye Curtis ambapo baadaye
walifarakana hivyo Nay akaamua kumchukua mtoto kutoka mikononi mwa mama
yake japo ilimletea shida mpaka akalazimika kwenda kupima DNA na Curtis.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment