Hatimaye tatizo la umeme lililotokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mnamo Machi 28 mwaka huu lapatiwa ufumbuzi baada ya umeme kurejea katika hali ya kawaida.

Katika taarifa iliyotolewa na  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili Aminieli Aligaesha jana ofisini kwake Jijini Dar es salaam , amesema kukosekana kwa umeme hospitalini hapo  kumetokana na waya mkubwa wa kusambaza umeme kupata hitilafu.

“Tayari waya umeshabadilishwa na kuwekwa waya mpya, mpaka sasa kazi imekamilika na huduma zinaendelea kama kawaida”alisema Aligaesha.

Aidha , Aligaesha alikanusha juu ya taarifa ya kifo cha mama mjamzito kuwa alikosa huduma akiwa katika chumba cha upasuaji kwasababu ya tatizo la kukatika kwa umeme .

“Napenda kutaarifu umma kwamba taarifa hii siyo ya kweli bali ni upotoshaji kwani kifo cha mama huyu kilitokana na sababu za kitaalamu”alisema Aligaesha.
Imeandaliwa na Jacquiline Mrisho