Mripublikan Donald Trump ameshinda katika majimbo yote matano yaliyofanya uchaguzi wa awali wa urais wa Marekani Jumanne.
Vituo vya televisheni vya Marekani vilibashiri ushindi wake ambao utampeleka karibu kuwa mgombea urais wa chama cha Republikan.
Bilionea Donald Trump ameshinda katika majimbo ya Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania, na Rhode Island.
Kwa upande wa chama cha Demokrat, waziri wa zamani wa mambo ya nje Bi Hillary Clinton ameshinda majimbo ya Delaware, Maryland, Connecticut na Pennsylvania.
Lakini seneta wa Vermont, Seneta Bernie Sanders, alishinda katika jimbo la Rhode Island.
Wachambuzi wa siasa za Marekani wanasema ushindi huo wa Bi Clinton utamfanya awe mgombea wa chama hicho hata kama atashidwa na mpinzani wake katika uchaguzi wa awali wa majimbo yaliosalia.
0 comments:
Post a Comment