NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

UEFA Miaka miwili baada ya goli la Koke, hatma ya Barca kutetea ubingwa ipo mikononi mwa Atletico

Akiwa na miaka 24 tu, Koke tayari ameshacheza michezo 250 akiwa na klabu hiyo ya Jiji la Madrid. Koke alianza kuitumikia Atletico akiwa mdogo kabisa na ngazi kwa ngazi, mechi baada ya mechi, amefanikiwa kuingio kwenye mioyo ya mashabiki wa klabu hiyo na kujiandikia jina katika historia ya klabu hiyo. Jina la Koke lilikuwa kwenye mdomo wa kila shabiki wa Atletico Madrid baada ya moja ya michezo muhimu zaidi katika historia ya kubwa ya Atletico. Ilikuwa April 9, 2014 wakati Barcelona ilipokwenda Vicente Calderon Stadium kucheza katika mchezo wa kuamua nani anabaki katika michuano ya ulaya. The Blaugrana walikuwa wakipewa nafasi kubwa pamoja na sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza, lakini Diego Simeone alikuwa na mipango mingine. Aliwaagiza vijana wake kuingia uwanjani kupambana na Barcelona kwa kumiliki mpira na kushambulia. Matokeo ya kujiamini kwake yalikuwa ni goli la dakika ya tano ya mchezo. Mbinu za Simeone ziliisadia timu yake na kufanikiwa kulinda goli lao mpaka mwishoni mwa mchezo na kufanikiwa kusonga mbele. Mfungaji wa goli la Atletico Madrid alikuwa Koke. Lilikuwa goli lake la kwanza na la mwisho katika michuano ya ulaya mwaka 2013/14 – ingawa alifanikiwa kutoa assits mbili katika kuisadia kuiweka Atletico kuwa miongoni mwa timu bora barani ulaya baada ya miaka 40. Wapinzani waliofuatia walikuwa Chelsea ambao walifanikiwa kuwatoa na Rojiblancos wakakata tiketi ya kuingia fainali waliyocheza dhidi ya wapinzani wao Real Madrid katika fainali iliyopigwa Lisbon. Leo Atletico Madrid wapo Nou Camp kucheza dhidi ya Barcelona katika hatua ile ile ambayo mara ya mwisho walipokutana, Je nini kitatokea? Muda utatoa majibu.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment