Ujumbe
wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo (Monusco) umeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi
wa Tanzania wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya udhalilishaji kingono.
Wanajeshi
hao wanaodaiwa kufanya vitendo hivyo vya kingono dhidi ya raia ni wale
wanaohudumu chini ya kikosi cha jeshi kilichopo Kijiji cha Mvivi karibu
na mji wa Beni ulioko jimbo la mashariki mwa DRC la Kivu ya Kaskazini.
Monosco imesema imetuma mara moja timu ya uchunguzi katika eneo hilo kubaini ukweli wa kashfa hiyo inayowakabili Watanzania hao.
Monusco
ilisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa iwapo itathibitishwa kuwa
wanajeshi hao walihusika katika unyanyasaji wa kingono ikiwamo dhidi ya
watoto.
Shutuma
hizo zinakuja baada ya wanajeshi wa Ufaransa na wa kutoka nchi nyingine
kutuhumiwa kuhusika katika udhalilishaji wa kingono katika Jamhuri ya
Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa (UN) umesema umesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wanajeshi kufanya unyama kwa wananchi wa nchi hizo.
UN walisema kinachosikitisha zaidi wanaofanyiwa vitendo hivyo ni watoto wadogo.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment