Naibu
waziri wa Habari, michezo wasanii na utamaduni ametimiza ahadi yake aliyoitoa
kwa Timu ya taifa ya Tanzania Twiga stars ya shilingi laki tatu kwa kila
mchezaji endapo watapata goli dhidi ya Zimbabwe.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam
wambura amesema kuwa anawapongeza vijana hao kwa moyo wa kujitoa na kutokata
tamaa jamba linalotia faraja na kuakisi mafanikio hapo baadae.
“wanza
nipende kuwapongeza kwa kutokata tamaa baada ya kufungwa 2-1 hapa nyumbani
nikakutana nanyi kuwatia moyo, mkaahidi kufanya vizuri haikuwa kazi rahisI
KUPATA Ushindi ugenini mmeonyesha moyo wa kujitoa sana
licha ya kuwa hakuna manufaa makubwa mnayoyapata ya kifedha, hongereni sana” alipongeza Wambura.
Wambura
aliwaasa wachezaji wa Twiga, kuwa mfano wa kuigwa katika jamiiili kuondoa dhana
kuwa watoto wakike wanaocheza mpira wa miguu hawana maadili jambo
linalokwamisha kwa kiasi kikubwa kididimiza mchezo huo nchini.
“tumerudi
kutoka Zimbabwe
na timu imetawanyika japo sio imetawanyika kabisa, hata huku mliko mnapaswa
kuendelea na mazoezi, na tubadili mitazamo sisi wenyewe kwanza kuwa mfano wa
kuigwa hii itasaidia wazazi kuruhusu watoto wao kushiriki mchezo huu
Watambue
kuwa watoto wote wa kie na wa kiume wanapaswa kucheza kwa hiyo kuwe na mgawanyo
wa kazi ili kutoa nafasi kwa watoto wote kucheza siyo wakimue peke yao ”. Alishauri Wambura.
Meneja
wa timu hiyo Furaha Francis, amewaomba wadau wamchezo huo kuwaunga mkono kwa
kuziwezesha timu zote za wanawake na wanaume, huku akishauri Serikali
kuzisimamia timu za taifa walau kwa 50% ili kulisadia Shirikisho la soka nchini
TFF ambalo wakati mwingine huzidiwa kutokana na kuwa na bajeti ndogo.
Kepteni
wa timu hiyo Amina Rashid, ameshauri kuanzishwa na kuboreshwa kwa ligi za soka
za wanawake ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara kuwa timu hiyo haifanyi
vizuri.
Naye
Mlinda lango wa timu hiyo Fatuma Omary amesemakuwa ni vema kuwekeza katika soka
la vijana wadogo wa kike ili kuwezesha upatikanaji wa wachezaji pale
wanapohitajika.
“kukiwa
na wachezaji wadogo waliandaliwa mapema hata tunapocheza sisi tunakuwa tunajuwa
baadae kuna wadogo zetu watakuja kushika na nafasi zetu sio kila siku Amina na
Fatuma wasipo kuwepo kocha anawaza ataziba vipi pengo lake”
Twiga
ilifungwa na Zimbabwe 2-1
jijini Dar es Salaam katika mechi ya awali na kisha kutoka sare ya bao 1-1
katika mechi ya marudiano iliyochezwa nchini Zimbabwe mapema mwezi uliopita
ikiwa ni mechi za kuwania kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment