Wananchi wa wilaya ya Kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina

Hayo yamesemwa leo na waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.
Mhe.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha Unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.

Naye mkuu wa wilaya ya Kyela, Dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya Malawi anatafutwa.

Matukio hayo yametokea mwezi Februari na Machi mwaka huu.
Wilaya ya Kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu Novemba, 2015 na hadi kufikia Machi, 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu.

Pia Waziri Ummy Mwalimu  ameahidi kuwapelekea dawa za kutibu maji (water guard) wananchi wa Kyela

Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini, takribani mikoa yote Tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi Agosti mwaka jana, isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi sasa.

Ripoti ya wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto ya Machi, 4 mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.

Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka, mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini kuongezeka.
Na Catherine Sungura, Kyela
403459e2-cbfc-4c35-9dce-581dcb27e11b
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na watendaji wa wilaya ya Kyela,kushoto ni makamu mwenyekiti wa wilaya, Stephen Mwangalaba na kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Thea Ntara.
b4857790-324f-434e-802b-1b2a52ef4269
Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Thea Ntara akizungumza na watumishi wa wilaya ya Kyela.
06407b43-0437-4793-be27-fddb99a54780
Baadhi ya wauguzi wa hospitali ya wilaya wakimsubiri kumpokea waziri wa Afya, Mh.Ummy Mwalimu amewakumbusha watoa huduma hao kuwahudumia wananchi kwa kufuata weledi wa taaluma zao.
0b711e3c-ce7e-4925-9e5b-aea741ee154f
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na watoa huduma wa hospitali ya wilaya ya Kyela.
290a0086-5fe6-4d75-9b53-8c56716a6966
Waziri Ummy Mwalimu akipata maelezo kwenye dirisha la wanaotumia kadi ya mfuko wa wa jamii( CHF) toka kwa mhudumu (hayupo pichani) wa hospitali ya wilaya ya Kyela.