Kama unataka kumpata mwanamke
unayemzimia bila tatizo lolote basi hakikisha unafuata taratibu hizi,
kwani utapata ujasiri wa kumtongoza mwanamke, kuanzia siku ya kwanza
hadi anapokuwa wako.
Hatua #1: Angalia ishara.
Ufunguo wa kutongoza ni kuzijua na kuzivumbua ishara kwa yale
anayofanya na kutenda, kuwa makini na stori ambazo anaeleza, mambo
ambayo anapenda kuongea na kila kitu ambacho kinaamsha hisia zake.
Kumbuka hapa unakuwa makini kwasababu ya mwanamke na wala si wewe hivyo
usijaribu kutoa maoni yeyote bila kufikiria madhara yake.
Hatua #2: Cheza na hisia zake.
Hapa jambo muhimu la kufahamu ni kuwa ni vyema uchague maneno matatu
yenye ushawishi ya kumwambia mwanamke, unaweza kubadilisha hisia zake na
akakubaliana na matakwa yako, Huu uwezo wa ‘kubadilisha’ hisia za
mwanamke ni jambo muhimu zaidi ya yote ikija katika maswala
ya kumtongoza mwanamke.
Hatua #3: Mpe uhakikisho.
Kila mwanamke (hata kama ni mrembo kiasi gani ama ‘amekamilika’ mbele
ya macho yako) huwa wana hulka ya kutojiamini ndani yao ambapo
kunahitajika kupewa uhakika kwa njia moja au nyingine. Hivyo, jambo
muhimu la kuzingatia wakati unampa uhakika ni pale ambapo utakuwa
mkweli.
Kumwambia
kuwa ana macho mazuri hakutasaidia; hii ni kwa sababu maneno kama haya
yashatumika mara kwa mara na kila mwanaume anatumia maneno hayo hayo.
Kumpongeza na kumpa na kumuhakikishia kwa jambo ambalo hajiamini nalo
kutamfanya akuthamini na kumuweka karibu na yeye zaidi na kama umefuata
hatua hizi mbili za kwanza vizuri basi hautakosa kupata jambo ambalo
litampendeza.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment