Na.Timotheo Lupembe
Kata ya
lukande iliyopo wilayani ulanga mkoani morogoro ipo mbioni kuondokana na kero
ya ukosefu wa shule ya sekondari ya kata
Akitoa
taarifa hiyo diwani wa kata ya lukande bwana Novatus majiji amesema kwamba kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 wanamkakati wa kuanza ujenzi wa shule ya sekondari ya
kata kwakuwa eneo la ujezi wa shule hiyo tayari limepatikana
Aidha bwana
majiji amesema ujenzi huo wa shule ya sekondari katika kata hiyo ukikamilika
utapunguza kero kwa wanafunzi ambao hivi sasa hulazimika kutembea umbali mrefu
kutoka katika vijiji vya lukande nagombe hadi kata ya mwaya kwa elimu ya
sekondari
Pia
amewataka wakazi wa vijijivya gombe na lukande kulipa kipaumbele suala hilo kwa
kujitolea katika shughuri za maendeleo ili kufanikisha
0 comments:
Post a Comment