Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali imejipanga kulitumia Jeshi la Magereza kuhakikisha Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda.
Lengo
hilo ni mkakati wa wizara kutaka kuendana na kauli ya Rais John
Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda kuelekea kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025.
Masauni
aliyasema hayo jana alipotembelea mradi wa kiwanda cha kokoto cha
Gereza la Msalato kilichopo Dodoma. Alisema Magereza ina rasilimali
nyingi ambazo zikitumika kikamilifu zinaweza kuifanya nchi kupiga hatua.
Alisema
kuna fursa nyingi ambazo jeshi hilo linaweza kuzitumia kufikia azma
hiyo, ikiwamo kuanzisha kiwanda cha viatu kwa ajili ya askari wa majeshi
mbalimbali.
“Inashangaza kuona majeshi yetu yananunua viatu kutoka nje wakati vinaweza kutengenezwa na Magereza. Lazima tujipange na ninaamini Jeshi la Magereza linaweza kuifanya kazi hiyo,” alisema Masauni.
Akizungumzia mradi wa kokoto wa gereza hilo, alisema zinahitajika Sh2.5 bilioni kwa ajili ya uwekezaji katika mradi huo.
“Inashangaza kuona majeshi yetu yananunua viatu kutoka nje wakati vinaweza kutengenezwa na Magereza. Lazima tujipange na ninaamini Jeshi la Magereza linaweza kuifanya kazi hiyo,” alisema Masauni.
Akizungumzia mradi wa kokoto wa gereza hilo, alisema zinahitajika Sh2.5 bilioni kwa ajili ya uwekezaji katika mradi huo.
Alisema
kiwanda hicho kikianza kazi kitakuwa na uwezo wa kukusanya mapato ya
Sh6.8 bilioni kwa mwaka. Alisema kuna namna mbalimbali jeshi hilo
linaweza kupata mtaji huo ikiwa ni pamoja na kuomba mkopo kwenye benki
za nchini, kuingia ubia na mwekezaji au kupata ruzuku kutoka serikalini.
“Nataka
Magereza watafute namna ya kupata fedha hizo bila kusubiri ruzuku
kutoka serikalini. Najua watapata fedha hiyo kwa sababu mradi huu ni
mkubwa na utalifanya jeshi hili kuongeza mapato,” alisema.
Masauni
aliongeza kuwa anataka kuona siku moja jeshi hilo linajiendesha kwa
kujitegemea kuanzia kwenye chakula cha wafungwa mpaka miundombinu yake.
Alisema
hilo litawezekana kama watawekeza kwenye viwanda. Mrakibu Msaidizi wa
Magereza, Patrick Nasola alisema mradi huo utaendeshwa na jeshi hilo na
kuwa watakuwa tayari kumuuzia mtu yoyote kokoto watakazozalisha.
Alisema
mradi huo ukianza kazi utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 15 za kokoto
kwa siku. Alisema changamoto wanayokabiliana nayo ni uhaba wa fedha kwa
ajili ya kutengeneza mtambo wao ambao sasa umeharibika.
“Walikuja
wataalamu katika eneo hili la Msalato kupima wakabaini kuna madini mawe
mengi na sasa tuna leseni 15 kwa ajili ya madini mawe. Mawe yaliyopo
hapa ni kama yale yanayotumika kutengeneza tiles,” alifafanua.
Nasola
aliongeza kuwa wataweza kuzalisha fedha nyingi kutokana na mradi huo
kwa sababu ni eneo kubwa ambalo kwa ujumla wake lina madini mawe ya
kutosha. Alisema wanatarajia kuuza zaidi kokoto ujenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Msalato utakapoanza.
Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Msalato, Steven Mwihambi alisema kokoto ni moja ya miradi inayofanyika katika gereza hilo.
Alitaja miradi mingine kuwa ni ufugaji, kilimo na utengenezaji wa samani. “Tutaanzisha
viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya mazao tunayozalisha kama vile
alizeti. Changamoto kubwa ni uhaba wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
mipango yetu,” alisema kiongozi huyo wa gereza.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment