NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

PICHA LUKUKI ZA MATUKIO BUNGENI DODOMA



 Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga ambaye alisababisha wabunge wanawake wa upinzani kutoka bungeni wiki iliyopita kwa madai ya kuwadhalilisha,akichangia hoja bungeni Dodoma jana, ambapo alieleza kwamba amekuwa akipata vitisho lakini ana imani Jeshi la Wananchi Tanzania lililowasambatisha waasi wa DRC Congo M23 litamlinda. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.


 Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema akichangia hoja bungeni wakati wa kujadili Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa



 Wabunge wakiingia bungeni Dodoma  leo.



 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akijibu maswali yaliyoulizwa na wabunge



 Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.



 Waziri wa  Nchi Ofisi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angelah Kairuki (kulia) pamoja na Naibu wake, Seleman Jaffo bungeni Dodoma.



 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akiwasilisha makadilio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 bungeni Dodoma leo

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment