Serikali imeeleza mkakati wa kuzirudisha shule 33 maarufu katika ubora wake ili ziweze kufanya vizuri kama ilivyokuwa zamani.
Mkakati
huo ulielezwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,
Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti yake
bungeni.
Alisema
shule hizo zilipokuwa nzuri zikitoa elimu bora, zilizalisha vipaji
vingi, akiwamo yeye aliyesoma katika mojawapo.Alisema katika awamu ya
kwanza, shule 33 zitakarabatiwa.
Alizitaja shule hizo kuwa ni Ihungo, Ilboru, Kilakala, Mwenge, Msalato, Mzumbe, Ngaza, Pugu, Same, Tabora Boys na Tabora Girls.
Nyingine
ni Azania, Jangwani, Kantalamba, Mpwapwa, Tosamaganga, Malangali,
Milambo, Nangwa, Kibiti, Minaki, Ifakara, Songea Boys, Ndanda, Kigoma,
Kibaha na shule za ufundi za Bwiru Boys, Ifunda, Iyunga, Moshi, Mtwara,
Musoma na Tanga.
0 comments:
Post a Comment