NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Serikali yaja na mkakati mpya kuongeza umeme nnchini

 

Katika kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme wa kutosha serikali imefanya mapitio ya ripoti ya kuendeleza nishati ya joto ardhi kwa lengo la  kuongeza uzalishaji mwingine  wa umeme ambao utasaidia kwa Watanzania kupata dira ya maendeleo  na kuongeza maendeleo ya uchumi wa Taifa .

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Nishati  na Madini, Prof. Sospeter Muhongo,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati  na Madini  Dk. Mhandisi  Juliana Pallangyo amesema  kuanzisha kwa umeme wa jotoardhi unaotokana na mwamba wenye joto unaochemsha maji yaliyoingia ardhini ambapo utasaidia kupunguza  kwa kiasi kikubwa uhaba wa umeme hapa nchini .

Aidha  maeneo yaliyolengwa  ni Manyara, Ngozi Ngorongoro, Kisaki Majimoto Mara na mengineyo ambapo mvuke wake ni  msafi  na hauna madhara  yeyote  ambayo huweza kutumika kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani , viwandani kilimo na dawa .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa ilianzishwa Desemba 2013 kwa madhumuni ya kusimamia na kuongeza maendeleo ya ya jotoardhi nchini ambapo kuzalisha megawaiti 200 ifikapo mwaka 2020 na mega waiti 500 ifikapo mwaka 2025 na 2033 itazalisha megaweti 800 .

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment