NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

TRA YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI WA CHINA

traMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekutana na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka China ambao wanatekeleza miradi mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kupeana elimu juu ya utekelezaji wa kipengele cha zuio kwenye kodi ya mapato kwa makandarasi walio na miradi ambacho kinamtaka kulipa zuio hilo kabla ya kulipa kodi mwisho wa mwaka.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya 14 kwa wafanyabishara hao Meneja Elimu kwa Mlipakodi (TRA) Diana Masalla amesema kumekuwa na mkanganyiko namna ya kutenganisha kipengele cha zuio na kodi ya mapato ambacho kinamtaka mkandarasi kutenga malighafi ambayo yanakatwa zuio asilimia 2 na utaalamu asilimia 5.

Masalla amesema kipengele hiki si kigeni kipo miaka mingi bali kinashindwa kueleweka miongoni mwa wahusika na kinazihusu taasisi za serikali zinapokea ruzuku hivyo ni vema kila mmoja akaelewa kabla ya kutekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment