NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Wasanii wa filamu wafanya misa ya kumbukumbu ya kifo cha Rachel Haule

ggg




Wasanii wa filimu nchini wakiongozwa na Odama, Ijumaa hii wamefanya misa ya kumbukumbu ya kifo cha msanii wa filamu Rachel Haule.

cccc
 
Wasaii wakiwa mbele ya kaburi la Rachel Haule
Wasanii mbalimbali kama Ray Kigogo, Odama, Esha Buheti Steve Nyerere, Sabrina Rupia, Maya Mrisho, Senator Msungu Richie Mtambalike, JohariChagula pamoja na Lamata walihudhuia misa hiyo ambayo ilitawala majonzi.

Kupitia instagram, Odama aliandika:

Kumbukumbu ya majonzi inaumiza sana moyo wangu, nilikupenda ila Mola kakupenda zaidi, Ni kweli sasa nazidi kuamini dunia hii ni matembezi wote tukumbukeni sala. Pengo la rafiki yangu kipenzi Rachel hakuna wa kuliziba… Sijui nisemeje… Hapa niko kwenye nyumba yako ya milele nashindwa kuvumilia…unajua jinsi gani ulikuwa wa umuhimu kwangu… kutoka moyoni nimekukumbuka Sana RACHEL wangu, Mbele Yako Nyuma Yetu, Mungu Ailaze Roho Yako Mahali Pema Peponi… Amina🙏

gggcc
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment