
Shuti kali la mbali kutoka kwa kiungo
hodari Luka Modric lilitosha kuipa ushindi Croatia mbele ya Uturuki
katika muendelezo wa michuano ya Euro, mchezo wa kundi D uliopigwa
kunako dimba la Parc des Princes jijini Paris.
Modric alifunga goli hilo mnamo dakika ya
41 huku timu yake ikitengeneza nafasi nyingi ambazo hata hivyo
walishindwa kuzitumia ipasavyo
Darijo Srna and Ivan Perisic walifanya kazi
kubwa sana lakini juhudi zao zilizuiwa na kipa wa Uturuki Volkan
Babacan, ambaye aliokoa kwa umaridadi wa hali ya juu.
Kwa matokeo hayo Croatia wanakaa kileleni
mwaka katika kundi lao ambalo linaundwa na timu za Uhispania na Jamhuri
ya Czech pamoja na Uturuki.
Croatia watapamba na Jamhuri ya Czech siku
ya Ijumaa huko St Etienne, wakati Uturuki watakuwa na kibarua kigumu
dhidi ya mabingwa wateteza Uhispania katika mji wa Nice.
Dondoo muhimu
Croatia wana rekodi ya kipekee katika michezo ya ufunguzi ya michuano hii. Wameshinda michezo minne.
Uturuki wamepoteza michezo yao yote minne
katika mechi za ufunguzi za michuano ya Euro (1996, 2000, 2008, 2016),
ikiwa ni rekodi mbaya kabisa katika michuano hiyo
0 comments:
Post a Comment