NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Alichosema Zitto kuhusu Serikali kuhamia Dodoma

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameunga mkono harakati za Serikali kutaka kuhamia Mkoani Dodoma mara baada ya Rais, Dkt. John Magufuli kutangaza azma hiyo mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, ameandika yafuatayo;

Katika kutekeleza dhana ya kuirudisha nchi katika misingi ya kuasisiwa kwake, katika kampeni zetu za uchaguzi wa mwaka 2015, tuliahidi kwamba, kama tungeshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, serikali ingehamia Dodoma mara moja. Aidha mgombea wetu wa urais aliahidi kwamba angekula kiapo cha urais mjini Dodoma.

“Tulienda mbali zaidi tukasema kwamba kulikuwa na haja ya kuzitawanya wizara katika mikoa mbalimbali ili kuiweka serikali karibu na wananchi na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika pande zote za nchi.

Katika kutekeleza hili, kwa kuanzia, tukaweka nia ya kuihamishia wizara ya kilimo mkoani Mbeya, Wizara ya Nishati na Madini mkoani Mwanza na Wizara ya Utalii na Mali Asili mkoani Arusha,”  ameandika Zittto.

Ni katika msingi huu wa kisera tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake sahihi na wa kijasiri wa kuhamishia serikali Makao Makuu ya nchi Mjini Dodoma. Uamuzi wa kuhamishia serikali Dodoma ulifanywa miongo mine iliyopita lakini serikali ya CCM ilishindwa kuutekeleza kwa visingizio mbalimbali.

 Nchi kadhaa zilizokuja kujifunza kwetu namna ya kuhamisha makao makuu zilikwishatekeleza uamuzi huu wa kisera bila kigugumizi. Nchi mojawapo ni Nigeria iliyohamisha makao makuu yake kutoka Lagos kwenda Abuja.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment